Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Gekul apelekwa kwa DPP

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amesema jalada la kesi ya tukio la ukatili inayomkabili mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul limefikishwa kwenye ofisa ya mashtaka ya Mkoa (DPP) ili kufikishwa mahakamani.

Katabazi amesema bado wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa watatu huku akibainisha kuwa kila mtu aliyetajwa kuhusiana na tukio hilo ataitwa na kufanyiwa mahojiano.

“Hadi sasa tunawashikilia watuhumiwa watatu ambao hatuwezi kutaja majina yao kwa sababu ya upelelezi ambao ukikamilika tutawafikisha mahakamani wakati wowote kuanzia sasa,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *