Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Aliyefariki baada ya send off, kuzikwa siku ya harusi yake

Aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa, Rehema Chao (37) ambaye amefariki kwenye ajali pamoja na mama yake mzazi wakitoka kwenye ‘send off’ wanatarajiwa kuzikwa Desemba 02, 2023 nyumbani kwao kijiji cha Nganyeni, Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro siku ambayo ilipangwa kwa ajili ya harusi.

Ajali hiyo ilitokea Jumatano Novemba 29 mwaka huu baada ya gari walilokuwa wamepanda, aina ya Toyota Raum, kugongana na Lori wakati Rehema alipojaribu kulikwepa shimo na kukutana na lori eneo la Kichwa cha Ng’ombe wilayani humo.

Rehema ambaye alikuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Sua mkoani Morogoro baada ya send off yake kuisha alianza safari ya kuelekea nyumbani kwao Marangu akiwa ameambatana na familia yake kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake ambayo ingefanyika mkoani Arusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *