Watoto wanaongoza kufanyiwa ukatili

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewaasa wazazi na walezi kuwajengea watoto uwezo wa kujitambua na kujilinda dhidi ya ukatili wa kijinsia kufuatia hatari ya matukio ya ukatili na unyanyasaji yanayoendelea katika jamii.

Senyamule ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo amesema kuwa kwa sasa watoto Wapo katika hatari zaidi ya kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Aidha Senyamule ametaja maeneo ya kupeleka taarifa ikiwa mtu amefanyiwa ukatili kuwa ni Kituo cha huduma za Afya, Dawati la jinsia na watoto kwenye jeshi la polisi , Afisa ustawi wa jamii, Serikali za mitaa na Kijiji pamoja na Mashirika ya huduma ya msaada wa Sheria.

Maadhimisho ya siku 16 za ukatili wa kijinsia huanza kuadhimishwa Kila ifikapo Novemba 25 na kilele chake huadhimishwa Disemba 10 huku yakiwa na kauli mbiu zenye jumbe mbalimbali ambapo kampeni ya Mwaka 2023 inasema “Nyumbani kwangu hakuna ukatili”, na dhamira ya kampeni hiyo ni kuwahamasisha wanajamii kukemea ukatili kuanzia Nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *