Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Diwani athibitisha mtoto kubakwa na muuza bucha

Wakati serikali, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla wakiendelea na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo matukio ya ubakaji na ulawiti, vitendo hivyo vinazidi kushamiri huku taarifa ya kituo cha sheria na haki za binadamu ikionyesha asilimia 90%ya waahusika wanofanya ukatili huo ni ndugu wa karibu,wanafamilia na majirani.

Diwani wa Kata ya Kolanddoto Musa Elias amekiri kutokea kwa tukio la kubakwa kwa mtoto huyo huku akitoa wito kwa jamii kuwalinda watoto hususani katika zama hizi ikiwa ni pamoja na kutokuamini majirani wala wageni wanaowafikia na kuwaacha walale na watoto.

Jambo FM imemtafuta kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magom,i ili kufahamu undani wa tukio hilo na nini hasa kimekwamisha mtuhumiwa wa kesi hiyo kufikishwa mahakamani, ambapo amesema anafuatilia suala hilo na atatoa taarifa hapo baadae .

Jambo Media itaendelea kufatilia na kukuletea kila kitakachojiri katika tukio hili mpaka hapo mtuhumiwa atakapofikishwa mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *