Mtoto abakwa na muuza Bucha

Fatma Issa, si jina lake halisi, tunafanya hivi kulinda maudhui na utu wa mtoto amepata pigo baada ya binti yake mwenye umri wa miak 9 anayesoma katika Shule ya Msingi Kolandoto kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile na kijana aliyetambulika kwa jina la Malugu Juma (41) mkazi wa kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga aliyekuwa akiuza bucha jirani na nyumba yake.

Akielezea tukio hilo bi Fatma amesema ilikuwa ni tarehe 29/9/2023 majira ya saa moja jioni alitoka nyumbani kwake na kwennda dukani kununua mafuta ya kupaka na sabuni na kumwacha binti yake huyo nyumbani lakini wakati anarudi alipotaka kuingia ndani alishangaa kukutana na binti mlangoni akikimbia huku akipiga kelele na alipoingia ndani alimkuta malugu ambaye hakumuacha nyumbani hapo akiwa mtupu hana nguo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *