
Muimbaji na Muigizaji kutoka nchini Marekani Halle Bailey amezua gumzo pamoja na mpenzi wake ambaye ni Rapa wa Marekani pia DDG baada ya kuweka picha mitandaoni zikiwaonyesha wamevalia kama Tupac na Janet Jackson.
Wawili hao wameweka picha hizo ikiwa ni wiki ya kusheherekea sikukuu ya Halloween inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe za mwisho wa mwezi wa 10.