Nyota ya mchezo kutoka Nigeria, Burna Boy ametaja sababu ya kutumia kipande cha J Hus maarufu kama “Mr Ugly” kwenye intro ya ngoma yake ya City Boys, inayopatikana kwenye albamu yake ya I TOLD THEM.

Burna Boy amefunguka kupitia mahojiano aliyofanya na Kiss Fresh, kuwa ametumia sehemu hiyo kama utangulizi wake kwani J Hus alikuwa akiwazungumzia wanaume weusi Waafrika ambao kipindi cha nyuma hawakuonekana wenye kuvutia kwa jamii, ilikuwa wadada wengi wanaweka picha za wanaume weupe kwenye vyumba vyao sasa imekuwa tofauti eeh, tumejipata.