
Madini aina ya Almasi yenye thamani ya zaidi ya Dola za kimarekani 635,000 sawa na Bilioni 1.7 yamekamatwa yakisafirishwa kinyume na utaratibu katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa habari katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza waziri wa madini, Antony Mavunde amesema madini hayo yamekamatwa Mei 18 Mwaka huu yakisafirishwa na raia wa kigeni yakiwa kwenye mabegi manne.

“Majira ya saa saba mchana maofisa usalama kwa kushiriana na Mamlaka husika walibaini utoroshwaji almasi hiyo yenye uzito wa karati 2729.82 yenye thamani ya Dola ya kimarekani 635,847.66 Sawa na Sh.bilioni 1.745 – Waziri Mavunde.
Katika hatua nyingine Waziri Mavunde amesema serikali imesikitishwa na kitendo hicho cha utoroshwaji wa madini hayo na na mpaka sasa uchunguzi wa kina wa tukio hilo unaendelea.

“Uchunguzi wa kina unaendelea ulbaini mtandao wa wanaohusika na utoroshaji kuwezesha hatua za kisheria dhidi ya wote, ikiwemo kufikishwa mahakamani, kutaifisha madini na kuwafutia leseni,” amesema Mavunde
Sambasamba na hayo mavunde amesema kwa mwaka wa fedha 2015 /2016 serikali ilikusanya billion 162 kutokana na biashara ya madini lakini kutokana na udhibiti mkubwa wa utoroshaji wa madini mwaka wa fedha 2024 /2025 mpaka mwezi mei serikali imekusanya shilingi billion 925 huku lengo ikiwa ni kufikisha tirion moja .