PUTIN, TRUMP HAWATAHUDHURIA MAZUNGUMZO YA KUTAFUTA AMANI NA ZELENSKY

Rais wa Urusi, Vladimir Putin hatahudhuria mazungumzo ya amani kati ya Taifa lake na Ukraine, yanayotarajiwa kufanyika jijini Istanbul Nchini Uturuki, licha ya wito kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.

Tqarifa kutoka Ikulu ya Kremlin jijiji Moscow imeeleza kuwa ujumbe wa Urusi badala yake utaongozwa na msaidizi wa Rais Putin, Medinsky.

Itakumbukwa kuwa, Zelensky hivi katibuni alisema atahudhuria mazungumzo hayo ya ana kwa ana na Putin, iwapo rais wa Urusi atakubali na kwamba atafanya kila awezalo kuhakikisha mkutano huo unafanyika.

Duru za kisiasa pia zinaarifu kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump pia naye hatahudhuria mazungumzo hayo, licha ya awali kudokeza kuwa angeshiriki iwapo Putin angekuwepo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *