WATATU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA UKATILI WA KIJINSIA, UBAKAJI

Watu watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa makosa mbalimbali ya ukatili wa kijinsia kwa watoto, ikiwa ni pamoja na ubakaji wa watoto na kuingilia kinyume na maumbile.

Akizungumza na waandishi wa Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema katika kipindi cha miezi miwili jumla ya kesi tatu za ukatili wa kijinsia kwa watoto zilizofikishwa Mahakamani zimewakuta na hatia watu hao na wote washtakiwa kuhukumiwa miaka 30 kila mmoja.

Mutafungwa amesema katika kesi ya kwanza la jinai namba 2904/2025 mshtakiwa Malimo Mathias Nguno (41) mkazi wa wilaya ya Kwimba alihukumiwa Machi 12, 2025 na mahakama ya wilaya Kwimba kwenda jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 13 mlemavu wa kusikia.

Mutafungwa amesema katika shauri jingine la jinai namba 31962/2025 mshtakiwa Iddy Renatus Makungu (30) mkazi wa kijiji cha Kinamweli, wilaya ya Kwimba alihukumiwa Aprili 8, 2025 na mahakama ya wilaya Kwimba kwenda jela miaka 60 baada ya kutiwa hatiani na mahakama hiyo kwa kosa la kumbaka na kumsababisha ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14.

Aidha pia amesema katika shauri la tatu la jinai namba 3610/2024 mshtakiwa Japhet Elias Mshashi (19) mkazi wa kijiji cha Mission, kata ya Nansio, wilaya ya Ukerewe, alihukumiwa Mei 7, 2025 na mahakama ya wilaya Ukerewe kwenda jela miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuingilia kinyume na maumbile mwanafunzi wa shule ya sekondari Bokongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *