Taasisi 269 za umma zinadaiwa jumla ya shilingi Bilioni 311.98 za madeni ya Watumishi, ikijumuisha Serikali kuu ya shilingi bilioni 274.8 sawa na asilimia 88.
Hayo yamebainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akisoma ripoti ya ukaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema, Mamlaka ya Serikali za Mitaa zinadaiwa shilingi bilioni 24.54 sawa na asilimia 8% na mashirika ya Umma shilingi Bilioni 12.64 sawa na asilimia 4%.

“Madeni haya ni ya mishahara, gharama za usafiri kwa Wastaafu na marupurupu mbalimbali, sababu kuu ikiwa ni ufinyu wa bajeti, ucheleweshwaji wa fedha na udhaifu katika usimamizi wa fedha za umma,” amebainisha Kichere.
Aidha, ameongeza kuwa mwenendo wa deni la Serikali hadi kufikia Juni 30, 2024 lilifikia kiasi cha shilingi Trilioni 97.36, kutoka shilingi Trilioni 82.25 mwaka uliopita, ambalo ni ongezeko la Shilingi Trilioni 15.10 sawa na asilimia 18%.
“Deni hili linajumuisha deni la ndani shilingi Trilioni 31.95 na deni la nje Shilingi 65.41
Kwa mujibu wa Tathmini ya Uhimilivu wa Deni ya Desemba 2024, deni la Serikali bado ni himilivu ambapo uwiano wa deni kwa pato la Taifa la ndani ni asilimia 41.1% na deni la nje kwa pato la taifa ni asilimia 23.6%,
Upo chini ya viwango vya juu vinavyokubalika ambapo ni sawa na asilimia 55%” amesema Kichere