Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wakazi 344 kujengewa nyumba kupisha bomba la mafuta

Serikali Inatarajia Kujenga Nyumba 339 Kwa Ajili Ya Wananchi Kama Fidia Kwa Watakaopisha Mradi Wa Bomba La Mafuta Ghafi La Afrika Mashariki (EACOP) Linalojengwa Kutoka Chongoleani Mkoani Tanga Hadi Kabaale-Hoima Nchini Uganda.

Mratibu Wa Kitaifa Wa Mradi Wa Bomba La Mafuta Ghafi La Afrika Mashariki (EACOP), Asiadi Mrutu Akizungumza Wakati Wa Kikao Kazi Cha Wataalam Cha Kujadili Kuhusu Zoezi Linaloenda Kuanza La Upimaji Mkuza Wa Bomba La Mafuta Amesema Hadi Sasa Nyumba 175 Zimekwisha Jengwa Sawa Na Asilimia 52 Na Kupewa Wananchi.

Mrutu Amesema Kati Ya Wananchi 344 Ambao Watapoteza Makazi Yao Katika Utekelezaji Wa Mradi Huo 296 Wamechagua Kujengewa Nyumba Na Kwamba Wananchi 9,799 Kati Ya 9,898 Sawa Na Asilimia 98.8 Wamelipwa Fidia Sh. Bilioni 34 Na Serikali Kwa Ajili Ya Kupisha Mradi Huo.

Aidha, Mratibu Huyo Amewaomba Wananchi Katika Mikoa Linalopita Bomba Hilo Kuwa Na Moyo Wa Kizalendo Kwa Kuruhusu Mradi Kutekelezwa Pasipo Vikwazo Vyovyote Hasa Vya Ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *