Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

TMA yatoa tahadhari uwepo wa El Nino Tanzania

Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania (TMA) imesema El Nino inatarajiwa kuwepo katika kipindi cha mvua za msimu wa vuli zitakazoanza kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu ambazo zitasababisha athari katika maeneo mbalimbali nchini.

Akitoa taarifa hiyo leo Jumatano Julai 19, 2023 Meneja wa Utabiri wa TMA, Dkt. Mafuru Kantamla amesema hadi kufikia sasa inaonyesha imefikia asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Dkt. Kantamla aliyataja maeneo ambayo yataathirika na mvua za El nino ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *