Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Hati ya uchunguzi kifo cha Tupac yatolewa

Jeshi la Polisi huko Nevada Marekani limethibitisha kuwa ndani ya wiki hii limetoa hati ya upekuzi kuhusiana na mauaji ya rapa wa Marekani Tupac Shakur kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea.

Wapelelezi walifanya upekuzi huo katika nyumba moja huko Henderson, Las Vegas ambapo Shakur aliuawa kwa kupigwa risasi Septemba 1996.

Jeshi la polisi halijatoa maelezo zaidi kuhusiana upekuzi huo unaotajwa kuwa ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusiana mauaji ya Tupac.

Aidha taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi kutoka Las Vegas imedokeza kwamba hiyo ni kesi ambayo haijatatuliwa na wanatumai siku moja wanaweza kuibadilisha.

Shakur alikuwa na umri wa miaka 25 alipouawa na tangu wakati huo hakuna mtu aliyekamatwa wala mtuhumiwa yeyote ambaye kizuizini hadi  sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *