RAIS SAMIA SULUHU ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1,548 KUADHIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 63 YA UHURU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Disemba 09, 2024 ametangaza msamaha kwa wafungwa 1548, ambapo wafungwa 22 kati yao wanaachiliwa huru tarehe 9 Disemba, 2024  na 1526 wanabaki Gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha wa Rais. 

Rais Samia ametumia Mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(a) – (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohusu kutoa msamaha huo huku akisema ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa hao watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

Sehemu ya taarifa hiyo iliyolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Daniel Sillo ni hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *