Mkali wa Afrobeat, Tiwa Savage amekanusha stori iliyokuwa ikivuma kwamba alimtishia 2face kifungo ikiwa angeamua kuachana na Annie mkewe akisema si ya kweli.
Tiwa Savage alisema hakusema kitu kama hicho na kwamba anadhani ni wakati muafaka wa kuweka rekodi hiyo sawa badala ya kukaa kimya.

Amesema, “Sijasema chochote kuhusu 2face na Annie. Kutajwa kwa jina langu kuhusu suala la jela haikuwa mimi kamwe, ilikuwa ni propaganda tu kutoka kwenye shimo la kuzimu.”
Hata hivyo alibainisha kuwa, “2face na Annie ni marafiki wazuri kwangu. Katika wakati kama huu, bora ninachoweza kuwafanyia ni kuungana nao katika sala na sio kutoa kwa maoni ya dharau.”