Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga (TAKUKURU) imewaonya watu wanaojitoa kwenye kugombea nafasi mbalimbali, na wale wanaofanya sherehe na mashabiki wa wagombea maarufu chawa na kuwataka kuacha kufanya vitendo hivyo kwani ni makosa ya rushwa kwa mujibu wa sheria.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 11 20, 224 na Mchunguzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilayani Kahama Mlamuzi Kuhanda wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu elimu ya kupambana na rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
“Kuna watu ni machawa wa viongozi wanapewa mikoba ya hela au wanatumiwa hela kwenye simu wananunua pombe huku akimsifia mgombea, hiyo ni rushwa,Tunawaonya na viongozi wanaopewa pesa wanajitoa kwenye uchaguzi nao wakae mkao wa kula na viongozi wanaofanya sherehe na kuwapeleka watu kwenye mbuga za wanyama hiyo ni rushwa” Amesema Kuhanda.
Kwa upande wake Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa wilaya ya Kahama Abdallah Urari amesema kuwa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa inasema anayetoa na kupokea rushwa wote ni wakosaji na kwamba wameweka mitego mingi kuwakamata watu hao.
“Sheria ya Takukuru inasema anayeomba na kutoa rushwa wote wana makosa hivyo sisi tunawachukulia hatua wote hatuangalii upande mmoja,tuna mbinu zetu za kuchunguza na ukibainika wote tunawakamata hata wale wanaosema unatuachaje” Amemesema Abdalah
Nao baadhi ya waandishi wa Habari waliopata elimu kuhusu Rushwa wakati wa uchaguzi wameiomba taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoa elimu kwa wagombea mbalimbali kupitia vyama vyao ili waache kutoa rushwa kwa njia ya kuandaa sherehe mbalimbali katika maeneo yao.