Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza lakamata magunia 80 ya mifuko ya plastiki

Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Luchelele iliyopo Wilaya ya Nyamagana Mkoani humo wamekamata jumla ya magunia 80 yakiwa na mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na serikali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema jeshi la polisi ndani ya mkoa huo lilipokea taarifa kutoka kwa wananchi hatua ambayo iliwawezesha kukamata mifuko hiyo ya plastiki pamoja na jumla ya watuhumiwa watatu.

Meneja wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Ziwa (NEMC) Jerome Kayombo amesema shehena iliyokamatwa ni shehena iliyokua na mifuko ya plastiki ambayo kwa mujibu wa sheria imekatazwa kutumika hapa nchini kwani ni mifuko ambayo haiozi na inaweza kuhatarisha usalama wa viumbe hai waliopo majini ikiwemo samaki na viumbe wengine.

Nae Diwani wa Kata ya Luchelele Vicent Lusana amewaomba wananchi wa eneo hilo kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kubaini matukio kama hayo pamoja na vitu ambayo vinaweza kuhatarisha usalama wa watu pamoja na mali zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *