Tyson Furry Kuzichapa Tena Disemba 21 Nchini Saudi Arabia.

Na Iddy Rasheed

Mpigana masumbwi kutoka nchini Uingereza Tyson Furry anajiandaa kwenda kukabiliana na bondia mwezake katika pambano la marudiano linalotegemea kupigwa December 21 katika jiji la Ryadhi nchini Saudi Arabia.

Katika mpambano wao wa kwanza Tyson Furry alipoteza lakini binafsi yake amedai kuwa moja ya sababu ya yeye kupoteza pambano hilo ni kwa sababu kabla ya mpambano mke wake alimpa taarifa kuwa ujauzito aliokuwa nao umetoka na hiyo ilimtoa kabisa mchezoni kiasi cha kupelekea pambano.

Lakini kwa sasa amekuwa akitizama pambano hilo ambalo ndiyo pambano lake la kwanza kupoteza katika maisha yake ya masumbwi mara kwa mara akiangalia ni kwa namna gani alipoteza pambano hilo na anajipanga barabara ili kuhakikisha anamuangusha Usyk mapema sana katika mpambano unaofuatia.

“Sina mengi ya kubadilisha kutoka pambano ambalo Usyk alishinda mwezi Mei. Nitaongeza bidii kidogo tu ili kushinda pambano hilo” alisema Mwingereza huyo.

Anapanga kutegemea mtindo wake wa kushambulia, akilenga kupiga na kudhibiti zaidi pambano. Fury alisema kuwa ataenda mbele, akipiga tu bila kurudi nyuma na analenga kumuangusha Oleksandr Usyk katika raundi ya tisa. Anaamini kwamba mchanganyiko wake wa jabs na kupiga sehemu za juu za mwili utakuwa muhimu kumvunja bingwa huyo wa Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *