Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Binti na mdogo wake wajiteka wawatapeli wazazi wao

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Flora Mshana (12) pamoja na mdogo wake France MShana (8) kwa tuhuma za kujificha na kudanganya kuwa wametekwa ili wazazi wao watume fedha.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea Julai 3, 2024 ambapo binti huyo anadaiwa kuiba Sh150,000 kisha kwenda kupanga chumba kisha kumpigia mama yake simu akidai yeye na mdogo wake wametekwa na mtekaji anahitaji fedha ili waachiwe.

Mutafungwa pia amesema mara baada ya kupokea taarifa hizo jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza lilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kuwapata watoto hao wakiwa salama huku wakiwa na simu, godoro na vyombo vingine vya matumizi ya ndani walivyonunua kwa kutumia pesa aliyoiba mtoto huyo.

Hata hivyo jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza limetoa wito kwa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao ili kutengeneza kizazi chenye maadili bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *