Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Moto Wateketeza Vibanda Vinne,22 Vyanusurika Kahama

Na William Bundala,Kahama

Jumla ya Vibanda vinne kati ya 22 vya wafanyabiashara wa nguo,viatu na vinywaji  vilivyokuwa katika jengo moja vimeteketea kwa moto majira ya saa 12 asubuhi Juni 20,2024 katika mtaa wa Kagongwa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza na Jambo Fm kuhusiana na tukio hilo Mkuu wa jeshi la Zimamoto na uokoaji Wilaya ya Kahama,Kamanda Stanley Lhwago amesema kuwa moto huo umetokea majira ya saa 12 asubuhi na kwamba uchunguzi wa awali unaonesha  kwamba ulisababishwa na hitilafu ya umeme kutokana na ubovu wa miundombinu ya nyaya zilizotumika kuunganisha umeme katika jengo lililokuwa na vibanda hivyo.

Naye mmiliki wa jengo lililokuwa lililoteketea kwa moto Bw. Simoni Masunga amesema kuwa hafahamu chanzo cha moto huo kwakuwa nyumba yake ilikuwa haina umeme kwani Luku ilikuwa imeisha na kuongeza kuwa wapangaji wake watatu ndiyo waliothiriwa kutokana na maduka yao kuungua huku wafanyabiashara walionusurika na ajali hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Kagongwa Bw. Michael Mayala amewashukuru wananchi kwa kutoa msaada wakutoa vitu ndani ya Vibanda hivyo na kutoa wito kwa wananchi kuwa na mawasiliano ya Jeshi la zima moto na uokoaji kwa ajili ya kutoa taarifa mapema kabla madhara hayajawa makubwa pindi matukio ya moto yanapojitokeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *