Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

CAG Alibaini Nini Mkoani Mara Kwa Mwaka wa Fedha 2022-2023?

Na Adam Msafiri, Ibrahim Rojala

Serikali mkoani Mara imemuagiza katibu Tawala wa mkoa huo kwa kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kufuatilia na kuhakikisha kinarejeshwa kiasi cha shilingi milioni 272 fedha zilizolipwa kwa mkandarasi mshauri ambaye ni NorPlan Tanzania bila kufuata utaratibu.


Maagizo hayo yametolewa Juni 19,2024 na Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi katika Baraza maalumu la madiwani Manispaa ya Musoma wakijadili hoja za Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali(CAG) na kwamba kiasi hicho cha fedha kilitajwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali tangu mwaka wa fedha 2020/2021.

Wakati huo huo Kanali Mtambi ameagiza kuundwa tume mahsusi ya kuchunguza malalamiko ya wananchi kuhusu kutoridhishwa na hali ya utolewaji wa huduma za afya katika hospitali mbalimbali za mkoa huo sambamba na kuagiza kuwa utekelezaji wa Taarifa ya Mdhibiti unakuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote vya kisheria vya baraza la madiwani.

“Tarifa ya Ukaguzi inaoesha kasoro mbalimbali kwenye usimamizi wa miradi ya maendeleo hususani katika taratibu za ununuzi na Mikataba,niwatake sasa waheshimiwa madiwani muhakikishe kuwa mnafuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi ya fedha katika maeneo yenu na pale mtakapobaini taratibu zinakiukwa msisite kuchukua hatua stahiki kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwangu ili niweze kufuatilia kwa karibu”amesema Kanali Mtambi

 Ripoti kuu ya ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2022-2023 iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG) kwa upande wa Mkoa wa Mara iliibua hoja Kadhaa;

Miongoni mwa hoja hizo ni pamoja na Sekretarieti ya Mkoa huo kufanya manunuzi ya bidhaa za huduma zenye thamani ya shilingi milioni mia moja tisini na nane laki tisa na tano na mia nne sitini na mbili bila idhini ya bodi ya zabuni kutoka kwa zabuni ambao haukudhinishwa na GPSA.

Kupitia Ukaguzi huo CAG pia alibaini uwepo wa vyeti vya malipo ya jumla ya Shilingi milioni 97 ikiwa ni sehemu ya malipo ya kazi zilizotekelezwa lakini fedha hizo hazikujumuishwa katika nyaraka za vipimo hiyo ikiwa ni kinyume na Kanuni ya 243(2) ya Sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2013.

Eneo lingine lililomulikwa Mkoani Mara kupitia Ripoti ya CAG ya mwaka wa fedha 2022-2023 ni pamoja na uwepo wa miradi ya Maendeleo ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo iliyotekelezwa bila kuibuliwa na Jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Butiama yenye thamani ya Shilingi milioni sitini na tisa na laki tano kutoandaliwa na kuwasilishwa kwa Mpango wa Utekelezaji wa Miradi ya CSR wilayani Butiama iliyo na thamani ya milioni 40.

Aidha CAG pia alibaini Uwepo wa Upungufu katika utekelezaji wa Miradi ya CSR wilayani Butiama ambapo Kampuni ya CATA Mining haikuwasilisha mpano wake wa uwajibikaji kwa Jamii na halmashauri haikuandaa muongozo na kutofanya ufuatiliaji.

CAG kupitia ripoti yake hiyopia  aliibua hoja katika Mikopo ya Vijana,wanawake na Wenye Ulemavu ambapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini uwepo wa Vikundi 75 katika wilaya ya Serengeti na vikundi 52 wilayani Musoma ambavyo vilipokea mikopo licha ya uwepo wake kutothibitishwa,hii ikiwa ni kinyume na kanuni za utoaji wa Mikopo kwa wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2019 inayomtaka afisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri kufuatilia uendeshaji wa vikundi na uwepo wake,urejeshaji wa mikopo,kuhakikisha mikopo inatumika kama ilivyokusudiwa na kuratibu mafunzo ya vikundi.

Sambamba na hilo,CAG alibaini mabadiliko ya miradi ambayo haikuidhinishwa na Kamati ya Kudumu ya Fedha, Mipango na Uongozi ambapo vikundi 30 wilayani Musoma  vilipata kiasi cha shilingi milioni mia moja themanini na tatu laki tatu hamsini na mbili elfu mia tisa na hamsini,Wilayani Tarime Jumla ya Vikundi 10 vilinufaika na kiasi cha shilingi milioni sitini na tisa,na kutoka wilayani Serengeti Jumla ya Vikundi vitatu vilipata kiasi cha shilingi milioni ishirini na tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *