Tanzania Yaidhinishiwa Ufadhili wa Dola Milioni 900 na IMF

Shirika la kimataifa la fedha (IMF) limesema bodi yake ya utendaji imeidhinisha ufadhili wa dola milioni 786.2 kwa Tanzania kuisaidia nchi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Shirika hilo la kifedha linakamilisha pia tathmini tofauti ya kuruhusu malipo ya dola milioni 149.4 kwa ajili ya msaada wa bajeti.

Taarifa ya IMF iliyotolewa Juni 20 mwaka huu imeeleza kwamba Mamlaka za Tanzania zina dhamira ya kuendelea kutekeleza mageuzi ya kudhibiti uthabiti wa kifedha, kuimarisha ufufuaji wa uchumi, kukuza ukuaji endelevu na shirikishi.

Katika miaka mitatu iliyopita, utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan ulifanya mageuzi mbalimbali ya kiuchumi kwa lengo la kurudisha ukuaji wa uchumi katika kiwango cha ukuaji wa pato la taifa la kabla ya janga la Covid wa asilimia 6 hadi asilimia 7.

IMF Limefafanua kuwa Mpango wa mageuzi ya uchumi wa Tanzania bado umeendelea kuwa imara, na kuongeza kuwa ukuaji wa uchumi uliongezeka mwaka 2023 baada ya kupungua mwaka 2022.

Uchumi wa Tanzania ambao unategemea utali, madini, kilimo na viwanda, umeendelea kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa yanayochochewa na kuongezeka kwa sekta ya huduma, kulingana na Benki ya Dunia na waziri wa mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo alisema wiki iliyopita kuwa ukuaji wa uchumi unakadiriwa kufikia asilimia 5.4 mwaka huu, kutoka asilimia 5.1 yamwaka uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *