Na Anastazia Paul,Simiyu
Wafanyabiashara katika mji mdogo wa Malampaka wilayani Maswa mkoani Simiyu wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani Maswa kuwasogezea huduma katika maeneo yao ili waweze kuzipata kwa urahisi na kulipa kodi zao pasipokuwa na usumbufu.
Wafanyabiashara hao wameyasema hayo hii leo Juni 7,2024 baada ya kutembelewa na Maafisa wa TRA kwa lengo la kuwapatia elimu ulipaji kodi kwa wafanyabiashara ambapo wameeleza kuwa kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali wa kilomita 35 kwa ajili ya kupata huduma za TRA.
katibu wa umoja wa wafanyabiashara Malampaka Noel Doto ameeleza kuwa changamoto hiyo ya umbali inasababisha wafanyabiashara kushindwa kulipa kodi kwa wakati na hivyo kujikuta wakilipishwa faini na Mamlaka hiyo.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, kaimu Meneja wa TRA wilaya ya Maswa Bw. Issac Mathayo ameeleza kuwa jitihada zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha wafanyabiashara wanafikiwa na huduma za TRA na hali itakayowawezesha kulipa kodi kwa urahisi.