Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

15.3% ya watanzania ndiyo wana Bima ya Afya

Takwimu zinaonesha kuwa hadi Septemba 2023 ni asilimia 15.3 tu ya Watanzania wote ndiyo wapo katika mfumo wa bima ya afya, NHIF 8%, CHF 6%, NSSF shib 0.3% na bima binafsi ni 1%.

Waziri wa Afya Ummy mwalimu ameeleza hayo wakati wa uwasilishaji wa mswaada bima ya Afya kwa wote bungeni Leo Novemba 1,2023.

Waziri Ummy ameongeza kuwa kuanzia miaka ya 2000 serikali ilianzisha utaratibu wa bima ya afya kwa mifuko ya bima ya afya ya umma na kampuni binafsi za bima ya afya, hata hivyo bado wananchi wengi takribani asilimia 85 wapo nje ya utaratibu wa bima ya afya kutokana na uhiari wa kujiunga na bima ya afya.

Muswada wa bima ya afya kwa wote uliowasilishwa bungeni leo unalenga kuimarisha mfumo wa ugharimiaji huduma za afya kupitia bima ya afya kwa wote ili kufikia lengo la huduma bora za afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *