Polisi wamesema takriban watu 10 wamefariki na wengine wanane kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa tatu kuporomoka katika eneo la Kirdasah lililopo mji mkuu wa Cairo Nchini Misri.
Kuporomoka kwa jengo hilo, si jambo la kawaida nchini Misri yenye watu milioni 107, ambapo ujenzi wa ubora umekuwa ukizingatiwa katika vitongoji vya mijini na vijijini kwa watu wa kipato cha chini.

Kirdasah ni mji wa tabaka la kati kusini-magharibi mwa Cairo, ambao unajulikana kwa vitambaa vyake vya kusuka kwa mikono, tasnia inayovutia wenyeji na watalii wa kigeni wanaofika kwa biashara.