Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anatarajia kutunukiwa cheo cha cheo cha mwisho cha Jeshi (Marshal), Juni 9, 2025.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia chapisho la Mtandao wa X (zamani Twitter) na Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mtoto wa Museveni.

Rais Museveni mwenye cheo cha Jenerali, ameiongoza Uganda tangu mwaka 1986 wakati alipochukua Mamlaka mikononi mwa Tito Okello na Milton Obote Julai 1985.
Cheo cha Marshal kwa mara mwisho nchini Uganda kilimilikiwa na Idi Amin Dada, ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka minane kabla ya kuondoshwa na majeshi ya Tanzania mwaka 1979.