KIM SAE-RON NYOTA WA FILAMU WA KOREA AKUTWA AMEFARIKI

Nyota wa Filamu Nchini Korea, Kim Sae-ron (24), ambaye aliwahi kuwa muigizaji mahiri wa watoto, akionekana kwenye Tamasha la Filamu la Cannes na kwenye Netflix amekutwa akiwa amekufa.

Kim Sae-ron, nyota ambaye kazi yake ya kuigiza ilikabiliwa na changamoto mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni, baada ya tukio la kuendesha gari akiwa amelewa, alipatikana amekufa nyumbani kwake Jumapili alasiri ya Februari 16, 2024.

Polisi wa Kituo cha Seongdong huko Seoul, wamesema umauti wa Kim uligunduliwa na rafiki yake ambaye alikuwa amemtembelea nyumbani kwake, huku wakidai uchunguzi wa awali unaonesha alijidhuru ingawa kulionekana kuwa na dalili za uhalifu.

Kim ni mmoja wa waigizaji wachanga waliowika nchini Korea Kusini na hakuwa ameonekana katika maonesho yoyote tangu alipokabiliwa na shutuma za kukutwa na hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa mwaka 2022.

Kifo chake kinaashiria mkasa wa hivi punde ulioikumba sekta ya burudani inayostawi lakini yenye shinikizo la juu la Korea Kusini kwa ukosoaji wa madhara ambayo inawaweka kwenye afya ya akili nyota wanaochipuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *