Baada ya staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz kuonesha kuumizwa na kukasirishwa na kile alichokieleza kuwa ni kitendo cha kampuni ya Ziiki kuzuia wimbo wa Kibango kutoka kwa Msanii Lava Lava kutoka siku ya leo na matokeo yake kupanga utoke mwezi Mei, kampuni ya Ziiki imejibu tuhuma hizo na kukanusha kufanya kitendo hicho.
Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni, Ziiki wamebainisha kuwa wimbo huo ulitumwa Aprili 16,2024 na wao (Diamond na timu yake) walitaka wimbo huo utoke Aprili 19,2024 kitu ambacho si utaratibu wao kwani kwa kawaida huwa inachukua wiki tatu tangu wimbo ulipowasilishwa hadi kutolewa.