Zambia shule zafunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu


Nchini Zambia shule zimefunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu baada ya kucheleweshwa kwa mara kadhaa kutokana na mlipuko wa kipindupindu, ambapo siku rasmi ya kufunguliwa kwa shule ilichelewesha kwa wiki tano kama sehemu ya hatua zilizochukuliwa kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo hatari.

wizara ya elimu kwenye taifa hilo imesema itafanya uchunguzi wa kina kutathmini  namana shule zilivyojianda kwa ajili ya ufunguzi.

Karibia watu 500 wameripotiwa kufariki tangu mlipuko huo kuthibitishwa mwezi oktoba mwaka uliopita, ambapo kando na Zambia, Nchi Za Tanzania, Msumbiji na Zimbabwe pia zimeripoti kuathiriwa na mlipuko wa kipindupindu.

Kwa mujibu wa serikali, Zambia imekuwa ikikabiliwa na mlipuko wa kipindupindu kwa miaka kadhaa, ambapo maambukizi ya hivi sasa  yakielezwa kuwa mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *