
Timu ya Yanga imetoa kikosi kinachoelekea D.R Congo kwenye mchezo wao wa tatu hatua ya makundi ya kombe la Klabu Bingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya TP Mazembe, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Disemba 14 2024.
Kwenye page ya Instagram ya Yanga wameandika ‘Kikosi kinachosafiri leo kuelekea nchini D.R Congo kwenye mchezo wetu wetu wa tatu hatua ya makundi #cafcldhidi ya TP Mazembe utakaochezwa tarehe 14.12.2024’.
Kikosi hicho kimehusisha wachezaji kama Djigui Diarra, Mshery, Bakari Nondo Mwamnyeto, Kibabage, Kibwana, Aucho, Mudathir, Pacome, Chama, Aziz Ki, Musonda,Clement Mzize, Prince Dube huku Jean Othos Baleke ameachwa nje ya kikosi cha safari ya Wananchi kuelekea Congo.