YANGA SC WAITIKIA WITO WA BODI YA LIGI, WASIMAMA NA ‘HATUCHEZI’

Klabu ya Yanga SC imethibitisha kupokea barua kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria kikao maalum cha kujadili masuala yahusuyo mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC, dhidi ya Simba na kwamba wametii wito huo, huku wakionesha msimamo wao kuwa hawatacheza.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa hii leo Juni 9, 2025 na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo imeeleza kuwa, wameshiriki kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za Bodi ya Ligi nchini jijini Dar es Salaam na kuwasilisha msimamo wao wa kutoshiriki mchezo huo mpaka pale matakwa yao yatakapotimizwa

“Baada ya majadiliano ya saa kadhaa, Viongozi wa Klabu waliwasilisha msimamo wa Klabu yetu kuwa hatutashiriki mchezo namba 184 uliopangwa kufanyika tarehe 15 Juni 2025, mpaka pale matakwa yetu tuliyoyawasilisha kwa maandishi kwao yatakapotimizwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *