Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wenye kaswende waongoza kwa kuwa na virusi vya UKIMWI

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika asilimia kubwa ya watu wenye magonjwa ya ngono wana maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango jumuishi wa kudhibiti UKIMWI, magonjwa ya ngono na homa ya ini uliofanyika jijini Dar es Salaam Waziri Ummy, amesema utafiti uliofanyika mwaka 2016-17 umeonesha ugonjwa wa kaswende ulikuwa mara tano zaidi kwa watu wenye virusi vya UKIMWI ukilinganisha na asilimia 0.8 na watu wasio na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Ameongeza kuwa wenye virusi vya UKIMWI walikuwa na dalili za kutokwa na uchafu na vidonda sehemu za siri kuliko wasio na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *