Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga imewahukumu kunyongwa hadi kufa Masele Lubinza na Mussa Toshaga baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Andrea Mayunga kisha mwili wake kuuzika ndani ya nyumba huku Mshitakiwa wa tatu Mahenda Toshaga akiwa huru baada ya ushahidi kutomtia hatiani.
Hukumu hiyo imetolewa leo April 10, 2025 kupitia shauri namba 2025-02262-0000-05006 na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga Mhe.Seif Kulita baada ya kusikiliza ushahidi wa Mashahidi sita wa upande wa Jamhuri waliokuwa wakiongozwa na Imaculata Mapunda.
Jaji Kulita amesema tukio hilo lilibainima Apri 2 katika kijiji cha Mwamashimba kata ya Lyamidati baada ya mzee huyo kuondoka nyumbani kwake March 28 kwenda senta ya kijiji chao ndipo hakurejea mpaka ilipobainika kuwa kutokana na mgogoro wa madai ya pesa alizokuwa akimdai Njile Nkilijilwa mama wa familia hiyo hali iliyomsukuma marehemu kwenda mahakamani ili aweze kupata stahiki yake.

Jaji Kulita amesema kuwa wakati mchakato huo wa wito wa Mahakama ukiendelea ndipo watu hao walimvizia akiwa anatoka senta ya Lyamidati na kumpiga na kitu kizito kisha kuufukia mwili wake ardhini ndani ya nyumba ya familia hiyo.
Kwa mujibu wa Ushahidi uliowasilishwa na kamanda wa jeshi la Jadi Sungusungu kata ya Lyamidati umeonesha kuwa march 28 alipkea malalamiko ya familia juu ya kupotea kwa ndugu yao baada ya kwenda senta na kutorejea licha ya juhudi walifanya kutozaa matunda.
Katika ushahidi wa shihidi wa pili ambaye ni kaimu mkuu wa upelelezi wilaya ya Shinyanga ambapo walifika kijijini hapo na kuwafanyia mahojiano watu hao na kukiri kuhusika na mauaji hayo kisha kuwapleka mahali walipokuwa wamemfukia marehemu
kisha juu yake kuanika mahindi.
Katika ushahidi mwingine uliwasilishwa kutoka kwa daktari wa zahanati ya Ihugi aliyeufanyia Vipimo mwili,huo ulionesha kuwa marehemu alifariki kwa kupoteza damu nyingi sehemu za kichwani na kukatwa sehemu za siri.
Baada ya kuwasilishwa kwa shahidi zote sita mahakama ikawatia hatiani washtakiwa wawili kati ya watatu kunyongwa hadi kufa huku Mahende Toshaga akiachiwa huru baada ya kutotiwa hatiani.
Kesi hiyo kwa upande wa Jamhuri ilikuwa ikisimamiwa na waendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Imaculata Mapunda,Mboneke Ndemubenya na nyamunyaga Magoto huku upande wa utetezi wakilishwa na mawakili wa kujitegemea Aigustino Ijani,Grace Egha na Emmanuel Lugamila.
Aidha katika mauaji hayo yaliyotkea March 28, 2024 mshitakiwa mwingine Samwel Toshaga aliweza kukimbia mara baada ya kutekeleza tukio hilo ambapo jitihada za kumtafuta zinaendelea atakapopatikana mkondo wa sheria uweze chukua hatua stahiki kwani kitendo kilichofanyika ni unyama na ukatili dhidi ya ubinadamu na haki za Binadamu.