Jumla ya Watumishi 15,288 walioondolewa katika utumishi wa umma kwa kosa la kughushi vyeti, wameshalipwa michango yao yenye jumla ya shilingi Bilioni 47.02 na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSSSF na NSSF kama alivyoelekeza Rais Samia Suluhu katika sherehe za Mei Mosi, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeeleza kuwa Watumishi waliokuwa wakichangia katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) walistahili kurejeshewa michango ya asilimia 5 na waliokuwa wakichangia NSSF, asilimia 10.