WANANCHI WALIA SHIDA YA MAJI SINGIDA, SUWASA YATOA UFAFANUZI

Na Saulo Stephen – Singida.

Wakazi wa Kata za Mughanga na Kindai zilizopo Manispaa ya Singida, wameilalamikia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Singida (SUWASA) kwa kutopata huduma ya maji katika maeneo yao kwa kipind kirefu ,bila ya kuwa na taarifa yoyote rasmi kutoka kwa mamlaka hiyo.

Wakizungumza na Jambo FM wananchi hao wametumia nafasi hiyo kupaza sauti zao kwa kutoa malalamiko Yao kuhusu tatizo hilo la upatikanaji wa huduma ya Maji ambapo wamesema tatizo hilo limeathiri maisha yao ya kila siku kutokana na ukosefu wa huduma hiyo katika maeeneo yao.

Wamesema, hali inapelekea wakina mama kamka usiku wa saa 9 au saa 10 kwenda kutafuta maji kwenye bomba ambalo lipo umbali mrefu na maeneo wanayoishi jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Aidha wameongeza kuwa kutokana na ukosefu wa huduma hiyo ya maji inawalazimu kununua dumu moja la lita 20 kwa bei ya Shilingi 500 hadi 700 kitu ambacho wanashindwa kukimudu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Kufuatia malalamiko hayo, kutoka kwa wananchi hao jambo FM, imefika katika ofisi za SUWASA mjini Singida lengo ikiwa ni kufuatilia na kupata ufafanuzi wa kina juu ya changamoto hiyo, na kufanikiwa kumpata Meneja wa Uzalishaji Maji na Usambazaji kutoka SUWASA, Mhandisi Elisha Kivuyo.

Kivuyo ametoa ufafanuzi juu ya hali hiyo iliyojitokeza kwenye maeneo yaliyoathirika na ukosefu wa huduma ya maji kisema hali hiyo imesababishwa na kuharibika kwa mota katika eneo la Liti lakini hata hivyo wameisharekebisha na huduma ya maji imeeanza kurejea katika baadhi ya maeneo ya kata hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *