Na Saulo Stephen – Singida.
Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na Taasisi ya JAI, sanjari na Biosustain Tanzania Limited Wametoa mkono wa Eid Al Adha kwa wagonjwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida Mandewa.
Wakiongea wakati wa kukabidhi Mkono huo wa Eid kwa wagonjwa hao viongozi kutoka Bakwata akiwemo katibu wa Bakwata mkoa wa Singida Omari Muna pamoja na Mkurugenzi wa Biosustain Limited Sajad Haidar wamesema lengo la kutoa vitu hivyo ni kurudisha kwa jamii lakini pia kuungana na watu wenye uhitaji katika katika kusherehekea sikukuu ya Eid kwa pamoja na kutoa fara kwa wagonjwa.

Miongoni mwa vitu vilivyotolewa kwa wagonjwa hao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa ni pamoja na chakula, Matunda mbalimbali, maji pamoja na Juice.
Kwa upande wake Muuguzi msaidizi kutoka Hospitali ya rufaa ya Singida, Tabita Crement Mkumbo kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ameshukuru taasisi hizo kwa kutoa mkono huo wa iddi kwa wagonjwa katika Hospitali hiyo.


