Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Vyandarua zaidi ya 200,000 vinatarajiwa kutolewa bure kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

Katika kupambana na ugonjwa wa malaria hapa nchini Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza inatarajia kugawa bure zaidi ya vyandarua laki mbili kwa wananchi wa halmashauri hiyo.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Malaria katika Halmashauri hiyo Abdurahman Mgonja ambapo amesema katika jamii bado mwitikio wa kutumia vyandarua ni mdogo hivyo ameitaka jamii kuwa na desturi ya kutumia vyandarua ili kukabiliana na ugonjwa huo wa malaria.

Mgonja pia amesema moja ya changamoto ambayo inapelekea kuwa na mwitikio mdogo wa kutumia vyandarua ni uwepo wa dhana potofu ya kuwa vyandarua vyenye dawa vinavyotolewa na Serikali husababisha madhara kwa watumiaji ikiwepo kueneza kunguni na kupunguza nguvu za kiume kwa akina baba jambo ambalo halina ukweli wowote.

Pamoja na hayo Mgonja amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaoenda kinyume na matumizi sahihi ya vyandarua hivyo ikiwemo shughuli za uvuzi, ufugaji na kilimo cha mbogamboga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *