VIONGOZI FANYENI KAZI KWA WELEDI, MALIZENI CHANGAMOTO ZA WANANCHI – NDUMBARO

Waziri wa Katiba na Sheria, Damas Ndumbaro amewataka viongozi mbalimbali wa Serikali hapa nchini kufanya kazi kwa weledi bila kujali Itakadi, hadhi au imani ya mtu, ili kumaliza changamoto zianazowakabili wananchi.

Mhe. Ndumbaro ametoa kauli hiyo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika katika viwanja vya Furahisha Wilayani Ilemela.

Amesema, maendeleo ya jamii hayataweza kufikiwa kama hakutakuwa na haki na amani akitolea mfano mataifa yenye migogoro ya ndani ambayo imesababisha raia wao kuhama na namna maendeleo yamekuwa duni katika mataifa hayo.

“Hakika kundi la wananchi wanyonge, wanaoishi pembezoni, ambao si rahisi kupata msaada wa kisheria na wasio na uwezo litakuwa limefikiwa kwa kiwango kikubwa, na wengi sasa hawatapoteza muda mwingi kushughulikia changamoto zao za kisheria bali watajikita katika shughuli za maendeleo,” ameeleza Mtanda.

Katika hatua nyingine Ndumbaro pia amesema Viongozi wa ngazi ya juu wana imani kubwa kwamba kupitia kampeni hiyo na elimu itakayotolewa, watendaji pamoja na wananchi watapata uelewa wa masuala ya kisheria, migogoro mingi iliyokuwepo katika ngazi za kijamii itatatuliwa na wananchi watapata huduma za msaada wa kisheria kwa urahisi na ufanisi.

“Hakika kundi la wananchi wanyonge, wanaoishi pembezoni na wasio na uwezo litakuwa limefikiwa kwa kiasi kikubwa na wengi sasa hawatapoteza muda mwingi katika kushughulikia changamoto zao za kisheria bali watajikita katika shughuli za maendeleo,” ameongeza Waziri Ndumbaro.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Alfredy Dede amesema Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imelenga kuhakikisha wananchi wanapata haki katika changamoto zote wanazopitia huku pia akisema kampeni hiyo itaendeshwa jijini Maanza kwa siku kumi katika sehemu zote za mkoa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *