VIKAO VYA KUCHUJA WAGOMBEA WA CCM VIKATENDE HAKI – DKT. SAMIA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza vikao vinavyoenda kuchuja Wagombea, vikatende haki.

Dkt. Samia ameyasema hayo hii leo Mei 30, 2025 katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao ulioanza Jana, Mei 29, katika ukumbi wa Mikutano Jakaya kikwete Jijini Dodoma, ambapo ameongeza kuwa usiwepo mwanya wa kupitisha wale wanaotafuta kukiharibu chama.

“Tukitoa Mwanya ndugu zangu, tukipitisha wanaotafuta na mimi niwemo ndio tutapata wale wanaokwenda huko chama kinakuwa Gwajimanaizi, kwa vyovyote vile tusigwajimanaizi chama chetu, Magwajima tuyaache nje, hamna kuoneana mtu aibu wala haya,” amesema.

“Anayefaa haambiwe na asiye faa tuseme huyu anakasoro moja mbili tatu hatufai kwa huko mbele tunako kwenda”. Amesema Dkt. Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *