Vifo vya wanafunzi Arusha waziri Mchengerwa atoa  agizo kwa wakuu wa wilaya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaelekeza maafisa elimu nchi nzima kuwaelekeza wakuu wote wa shule na walimu wakuu kwenye maeneo yao kuwaangalia wanafunzi hususani katika kipindi hiki cha mvua ili kuepusha majanga yanayoweza kuepukika.

Waziri mchengerwa ametoa kauli hiyo mapema leo April 13, 2024, ikiwa ni siku moja tu tangu kutokea kwa ajali ya gari la shule ya msingi Ghati Memorial Arusha inyodaiwa kusababishwa na ukaidi wa dereva wa gari hilo aliyediriki kukatiza katika mfereji wa maji na kusababisha gari kusombwa na maji hatua iliyo sababisha vifo vya wanafunzi.

Kufuatia ajali hiyo Waziri Mchengerwa ametoa pole kwa shule na familia kufuatia kuondokewa na wanafunzi hao katika mazingira yanayo ashilia uwepo wa uzembe ambao ungeweza kuepukika.

Waziri Mchengerwa amesema katika kipindi hiki cha mvua ni vyema Wakuu wa wilaya wakisisitiza ulinzi wa Watoto kwenye maeneo yao kuanzia kwa maafisa elimu wa wilaya na kata, walimu, wazazi na walezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *