Tutumie michezo kuendeleza amani, usalama na utulivu – Rc Mtanda

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Said Mtanda leo Aprili 13, 2024 amezungumza na viongozi wa matawi ya Yanga kutoka Mikoa ya kanda ya ziwa na kuwakumbusha kutumia michezo ili kudumisha amani, usalama na utulivu hapa nchini.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye ni mkereketwa wa timu hiyo amesema viongozi hao licha ya kuwa na dhamana ya kuhakikisha timu yao wanaipa nguvu ya kiuchumi lakini usalama na amani ni jambo la muhimu sana.

“Hakikisheni kwenye matawi yenu mnakuwa na wanachama hai lakini pia waliostaarabika kwa kuwaheshimu viongozi wao na hata wanapokuwa viwanjani,” Mkuu wa mkoa.

“Mimi ni mwanachama mwenzenu lakini pia ni Pamba Jiji FC tushikamane kuhakikisha inapanda ligi kuu msimu ujao,tumebakiza michezo mitatu tunahitaji nguvu zaidi kuliko wakati wote,” amesisitiza mkuu huyo wa mkoa.

Kuhusu umuhimu wa wanachama ndani ya klabu, Mtanda amewataka viongozi hao kuhakikisha wanaleta mageuzi chanya ya kiuchumi kwani ndiyo mtaji wa klabu.

Mkurugenzi wa masoko,matawi na wanachama kutoka makao makuu Ibrahim Samwel amebainisha mkutano huo ni sehemu ya mikakati ya klabu ya Yanga kuhakikisha wanachama wanashiriki kikamilifu kuimarisha klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *