
Frank Aman, Geita.
Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (Osha) wamendesha Mafunzo ya Usalama Mahala pa Kazi kwa Wachimbaji wadogo hususani Wanawake pamoja na kuwapatia Vifaa vya Usalama Mahala pa Kazi (PPE) zaidi ya 50 zitakazo weza kuwasaidia Wanawake wanaojihusisha na Shughuli hizo za Uchimbaji katika kuadhimisha Wiki ya Mwanamke Duniani.
Hayo yameelezwa na Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Uendelevu wa Kampuni ya GGML, Gilbert Mworia wakati akikabidhi Vifaa hivyo kwa Vikundi vya Wachimbaji wadogo Wanawake zaidi ya 50 ambao wengi wao hufanya shughuli hizo za Uchimbaji katika maeneo hatarishi hususani maeneo yanayokuwa na Vumbi zenye mchanganyiko wa Kemikali hatarishi zinazoweza kusababisha Magonjwa kama vile Kifua Kikuu.
Akizungumza wakati wa utoaji wa Vifaa hivyo, Meneja Mwandamizi Idara ya Afya, Mazingira na Mafunzo GGML Dk. Kiva Mvungi amesema kuwa Wachimbaji wengi wako katika Mazingira hatarishi kupata Magonjwa ikiwemo Kifua Kikuu, hivyo kupatiwa Vifaa hivyo kwa Vikundi vya Wanawake Wachimbaji wa Mgodi huo utawasaidia kujiepusha na Magonjwa yanayohusiana na Mfumo wa Upumuaji.
Kwa upande wake, Mkaguzi wa Afya Mwandamizi kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Amina Shilamangu amesema kuwa wameamua kutoka Mafunzo ya Elimu ya Afya Mahala pa Kazi kwa kuwa Wachimbaji hao ambao wako katika hatari ya kupata Magonjwa hatarishi kama vile Kifua Kikuu kutokana na Vumbi wanalovuta wakati wakiendelea na Shughuli zao za Uchimbaji.
Pia amewaasa Wachimbaji hao kuendelea kuzingatia Masuala ya Usalama Mahala pa Kazi ambapo kupitia Mafunzo hayo yaliyotolewa kwao Wachimbaji waliopo katika Maeneo mbali mbali ya Migodi Mkoani humo ambao kwa ujumla wake wanafikia 280 kwa Mkoa wa Geita pekee.