Jeshi la polsi mkoa wa Shinyanga limekamata vipodozi vyenye viambata sumu pamoja na vifaa tiba ikiwa ni pamoja na dawa za binadamu ambazo ni mali ya serikali zikiuzwa holela katika maduka ya madawa ya watu binafsi katika kata ya segese halmashauri ya msalala wilayani kahama ambayo hayaruhusiwi kuuzwa kwa watu binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Octoba 12 2023 kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Acp Janeth Magomi amesema dawa vifaa tiba na vipodozi hivyo vyenye viambata sumu vimekamatwa katika msako uliofanywa na jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na mamlaka ya vifaa tiba na dawa ( TMDA).
Katika hatua nyingine Magomi amesema katika msako unaoendelea kufanywa na jeshi la polisi wamekamata viroba vitano vya mifuko ya plasick ambayo imepigwa marufuku hapa nchini pamoja na mirungi bunda 20,bangi gramu1800 na lita tano za pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo.