Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

VIDEO: Watumishi waliomwagiana Drip wasimamishwa kazi

Watumishi watatu katika Hospitali binafsi ya Sakamu iliyopo Mji wa Geita Wilaya na Mkoa wa Geita wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kufuatia video fupi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha watumishi wawili wakimpongeza mwenzao kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa huku wakimwagia Maji kwa kutumia majitiba maarufu ‘dripu’.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dkt. Salvatory Msimu wakati akizungumza na Wandishi wa Habari waliofika katika Hospitali hiyo ambapo amekiri tukio hilo kutokea kwenye hospitali yake na sio kwenye kituo cha afya cha Nyankumbu kilichokuwa kikidhaniwa awali.

Dkt. Salvatory amesema baada ya video hiyo kusambaa walifuatilia na kubaini waliokuwa wakipongezana ni watumishi katika hospitali ya Sakamu hivyo mpaka sasa wamewasimamisha kazi watatu kupisha uchunguzi ili kubaini wale wote waliohusika katika tukio hilo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Jafari Mfano amewataja watumishi hao watatu waliosimamisha ni Elias Innocent Fundi Sanifu Dawa, Sada Suleman Muuguzi na Hawa Omary ambae pia ni Muuguzi lkatika hospitali hiyo ya Sakamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *