Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ametoa muongozo wa namna ya kuwasiliana na ofisi yake ambapo ametaja hadharani namba zake za Simu ya mkononi.
Muongozo huo ametoa wakati alipokutana na Wawekezaji wa Mashamba wa jiji la Arusha ambapo amesema ni vyema akatumiwa ujumbe wa maandishi kwenye namba zake kuliko kupigiwa.
Aidha ametaka wananchi wote wenye malalamiko ya migogoro ya ardhi au suala lolote kuhusu sekta ya Ardhi analotaka limfikie Waziri wa Ardhi atumie Ofisi za Makamishna Wasaidizi wa Mikoa katika mikoa waliopo.