Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema ana mashaka na Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo utakaotumika katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa leo.
Kocha huyo amesema uwanja huo sio rafiki kama ilivyo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na Chamazi hivyo hajui kama utawapa nafasi ya kucheza jinsi walivyozoea.
Amesema hajui ubora wa uwanja utakaotumika na kuongeza kwamba kiuhalisia haupo katika ubora kama uwanja wa Chamazi au kwingine, kwahiyo kuna uwezekano wasicheze kama ilivyozoleka lakini lengo lao ni kushinda.
Katika hatua nyingine Gamondi amesema licha ya kukosa muda wa kutosha kufanya maandalizi ya mchezo huo amewaandaa wachezaji wake kisaikolojia kutoa furaha kwa Wananchi.
‘Tumetoka kucheza michezo mingi, Jumamosi tumetoka kwenye mchezo wa derby, na tulihitaji mapumziko. Siwezi kuzungumza sana kuhusu maandalizi, tulipaswa kutoa mapumziko kwa wachezaji lakini tutapambana kwa ajili ya Wananchi”.
Yanga Sc itakutana na JKT Tanzania ambayo inasaka ushindi kwa kwanza katika ligi kwa kipindi miezi zaidi ya mitano, mara ya mwisho kushinda mchezo wa Ligi Kuu ilikuwa ni Novemba 03, 2023 walipoifunga Mtibwa Sugar 2-1.
Contact Us
P. O. BOX 71, Shinyanga, Tanzania
+255 766 408 253
info@jambofm.co.tz