NILIPOKEA URAIS NCHI IKIWA KWENYE MAZINGIRA MAGUMU – RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema alipokea Urais wakati Nchi ikiwa kwenye mazingira magumu kutokana na maradhi ya UVIKO -19 huku giza la kuondokewa kwa aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Mei 31, 2025 jijini Dodoma, baada ya kukabidhiwa tuzo maalum iliyoandaliwa na Bunge la Tanzania na kuongeza kuwa, pia mazingira ya kisiasa hayakuwa na sawa kwani ilikuwa ni muda mrefu tangu kumalizika kwa uchaguzi wa 2020.

“Wakati naipokea nchi, mazingira ya kiuchumi hayakuwa vyema kwa ulimwengu mzima kutokana na maradhi yale ya Covid 19, mazingira ya kijamii yalikuwa na fadhaha kubwa, kwanza ya maradhi, lakini fadhaha ya kuondokewa na mpendwa wetu Rais aliyekuwa Madarakani, na mazingira ya kisiasa hayakuwa na bashasha kwa kuwa haikuwa muda mrefu tangu tumemaliza uchaguzi wa 2020,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *