UKIJENGA URAFIKI NA TUFAA HUTAMUHITAJI DAKTARI

Tufaha ni tunda la kitropiki linalojulikana kwa ladha yake yenye kuburudisha na huwa lina rangi tofauti kulingana na mbegu au aina ya eneo linapolimwa ikiwemo nyekundu, nyeupe, na kijani.

Tufaa sio tu lina ladha lakini pia ulaji wake yaani kula tunda moja la tufaa kila siku humfanya mtu asiwe na haja ya kuonana na daktari.

Tufaa pia hutumika katika kudumisha afya, kukinga na kutibu magonjwa mbalimbali mwilini kiasi mtu huwa imara na mwenye uhakika.

Tufaa lina Vitamini K, na nyuzinyuzi za chakula pamoja na dawa-lishe (phytochemicals), aina ya quercetin flavonoid.

Zifuatazo ni faida za Tufaa katika mwili wa mwanadamu.

  1. Matufaa ni tiba nzuri ya ugonjwa wa kuharisha.

2. Husaidia katika matibabu ya uvimbejoto wa utumbo (colitis)

3. Husaidia katika matibabu na kuzuia shinikizo la damu

4. Husaidia katika tiba na kuzuia magonjwa ya mzio (allergy) pamoja na pumu ya mapafu.

5. Hutibu tatizo la kupata choo kikavu au kutokupata choo (constipation)

6. Ni dawa nzuri sana kwa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

7. Husaidia katika matibabu na kuzuia mawe katika figo.

8. Hupunguza hatari ya kupata saratani ya mapafu, saratani ya utumbo na ugonjwa wa kisukari.

9. Huimarisha afya ya ini.

10. Husaidia figo kuondosha sumu aina ya uric acid ndani ya damu.

Kwa ajili ya tiba kula matufaa kiasi cha kilo mbili kila siku kwa muda wa siku saba mfululizo.

Kunywa juisi ya matufaa bilauri moja kila baada ya saa nane kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *