UFAHAMU MCHAICHAI NA FAIDA ZAKE, NI KINGA YA SARATANI

Bila shaka wengi wetu tunaufahamu mmea ambao ni kiungo cha Chai unaofahamika kama MCHAICHAI, wengi wanautumia na kuufahamu kama kiungo cha chakula jikoni na wengine hutumia kama dawa ya mbu.

Lakini, suna hakika unafahamu kuwa majani haya yana faida kubwa kiafya na Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda vinavyotengeneza manukato na sabuni.

Kwa mujibubwa tafiti mbalimbali, zinaonesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari za maradhi mbalimbali ya tumbo, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda.

Hata hivyo, wengine huamini kuwa, mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na misuli.

Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya
mchaichai inasaidia kupunguza
joto kwa mgonjwa mwenye homa.

Hapa nakuletea faida nyingine za mchaichai kiafya, ambazo zitakufanya upate utaalam ama wa kukusaidia au kuwasaidia wengine.

KINGA YA SARATANI.

Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani.

Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka
Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza
kusababisha saratani.

MMENG’ENYO WA CHAKULA.

Husaidia umeng’enyaji wa chakula na Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu
magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.

Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini ambapo Katika matibabu,
unatibu magonjwa mengi ikiwemo
kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali.

KUSAFISHA FIGO.

Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu
mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali
kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha
magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.

Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika
kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati
mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.

MAUMIVU WAKATI WA HEDHI.

Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama
chango.

Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi.

MCHAFUKO WA DAMU.

Vilevile mchaichai una kazi ya kusafisha damu, hasa kwa watu ambao wamekuwa na
tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutoka majipu.

KUZUIA KUHARISHA.

Mchaichai pia unaelezwa kuwa ni dawa ya kuzuia kuharisha ambapo una uwezo wa
kupambana na mdudu aina ya protozoa anayesababisha ugonjwa huo.

WAJAWAZITO.

Endapo mjamzito atatumia majani ya mmea huu kwa muda mrefu, ataweza kujiepusha
kujifungua kwa njia ya upasuaji kwani husaidia katika kulegeza nyonga ambazo hubana katika kipindi cha ujauzito na kufanya
njia kuwa ndogo kuwezesha mtoto kupita.

VIDONDA VYA TUMBO.

Kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na
vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia
kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.

HUONGEZA CD4.

Kwa wagonjwa wa ukimwi, mchaichai unaelezwa kuwa huongeza CD4 na inashauriwa kuwa ni vyema mgonjwa wa
aina hiyo akapendelea kutumia zaidi mchaichai kuliko majani ya chai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *